Duration 3:36

Matobosha ya Nazi

245 watched
0
12
Published 2 Apr 2020

Leo nimepika matobosha ya Nazi , natumai utafurahia kupika kwako na resipe yangu. Kipimo cha nusu (½kg) Unga ngano ½kg Sukari 1½cups Iliki 1tbsp Maji 3cups Tuwi la nazi 3cups Chemsha maji 3cups, iliki 1tbsp na sukari ½cup kwa dakika 10. Weka unga ngano;kampuni upendayo (Ajab/Dola) nusu, chemsha. Koroga mpaka ushikane;usiwe mwepesi wala nzito. Weka kwa sinia kubwa unga upoe,toa shepu ya vijidondo. Chemsha sukari 1cup, iliki 1tbsp na tuwi la nazi 3cups kwa dakika 10.(itakua bora ukitumia sufuria ulochemshia unga ili ipate ladha nzuri) Weka vijidondo vyako kwa sufuria acha dakika 10 au 15 ipate kuiva. Puwa matobosha yako yakiwa majimaji kwa sababu yakipoa yanakua rojo rojo. Ni vizuri pia kupuwa majimaji kiasi na uwache yapowe kabisa. Alafu weka kwa vibakuli vyako na tayari kuliwa . 😋😋😋 I love you all ❤️. Like. Share. Comment. Subscribe.

Category

Show more

Comments - 2