Duration 36:59

SIMBA SC 1-1 UD SONGO: FULL HIGHLIGHTS (CAF CL - )

800 320 watched
0
1.8 K
Published 25 Aug 2019

Wekundu wa Msimbazi Simba SC wameangukia pua kwenye Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na UD Songo ya Msumbiji na kutupwa nje ya michuano katika hatua ya awali. Simba imeyaaga mashindano hayo kufuatia matokeo ya sare ya bila kufungana iliyoyapata katika mcheo wa kwanza uliopigwa wiki mbili zilizopita nchini Msumbiji, na hivyo wapinzani wao UD Songo kufuzu raundi ya kwanza kwa faida ya bao la ugenini. Katika mchezo wa leo uliopigwa kwenye Dimba la Taifa Dar es Salaam, wageni Songo ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 14 kwa free-kick kupitia kwa nahodha wao Luis Misquissone. Simba waliongeza kasi ya mashambulizi na umiliki wa mpira huku wakifanya mabadiliko kadhaa na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati lililofungwa na Erasto Nyoni dakika ya 87 baada ya Miraji Madenge kuangushwa ndani ya eneo la hatari. Mara baada ya mchezo Msemaji wa Simba Haji Manara ameomba radhi huku akisema yuko tayari kuwajibika.

Category

Show more

Comments - 280